Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

FEROUZ AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA

Posted in
No comments
Tuesday, January 14, 2014 By Unknown

Vijana ni nguvu kazi ya taifa, lakini vijana hao hao wanaweza kuwa 

chanzo cha taifa kutoendelea na kubomoka. Ubomoaji wa

taifa huwa kwa namna 

nyingi ikiwemo uvivu, ufisadi, na kadha wa kadha. Lakini hapa, tuangalie
 hili la madawa ya kulevya na bangi.
Kila kukicha kuna wasanii wa 
maigizo na filamu ambao 
tunasikia wamekamatwa na 
madawa ya kulevya, "unga" 
katika
 jitihada za 'kusaka 
maisha', wenyewe wanasema 
kuna ajali kazini. Wasanii hao 
ambao wengi ni vijana, na 
pale wanapoonekana kwenye 
runinga huwa hamasa
 kwa wadogo zao na jamii 
kwa ujumla, wakipenda kuwa 
kama wao.

Na mchana huu, maeneo ya Sinza, kuna taarifa ya mwanamuziki 
aliyetamba kwenye muziki wa bongo fleva, Ferouz, sanasana kwa wimbo 
wake wa Starehe, ambao ulikuwa ukionyesha madhara ya UKIMWI na 
virusi vya UKIMWI. Ferouz anadaiwa kukutwa na bangi, na picha ambazo 
Gospel Kitaa 
imezipata eneo la tukio, zinamuonyesha akisindikizwa na maafande 
kunako
mbele ya vyombo husika.

Vijana wa Tanzania tuna shida gani? 
Kama ni ardhi tunayo, kama ni nguvu 
tunazo, sasa nini shida zaidi? Ipo 
haja ya Operesheni ambazo Askofu 
Sylvester Gamanywa ameitisha za 
Takasika iliyomalizika hivi karibuni, 
na kisha kupokelewa na Operesheni 
Milikisha, kuwahusisha pia wasanii 
wa aina zote, maana wanaonekana 
kukumbwa na janga hili kwa sana, 
vinginevyo, vijana ambao ndio 
nguvu kazi ya taifa watakuwa wakijaa 
jela za ndani na nje, wakiacha wageni kuja kutawala.


Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.