HAYA NDIYO MAJIBU YA MWIGULU NCHEMBA KWENDA KWA WANAOPONDA UTEUZI WAKE,AWEKA WAZI ELIMU YAKE
Posted in
No comments
Wednesday, January 22, 2014 By Unknown
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwigulu Nchemba, ambaye jana alikuwa miongozi mwa manaibu waziri walioapishwa na Rais Jakaya Kikwete kushika nyadhifa zao amewaambia watu wanaoponda uteuzi wake kuwa hana haja ya kubishana nao kwani hawamjui.
Katika maelezo yake, Mwigulu alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumwamini kuwa anaweza kumsaidia katika kusimamaia sera na mipango ya fedha nchini. Watu wasionifahamu wanadai mimi sina viwango vya kufanya kazi hii; naomba wafahamu kuwa mimi ni msomi mwenye shahada ya ya pili ya uchumi na hivi sasa niko katika masomo ya kupata shahada ya uzamivu.
Mwigulu aliendelea kusema “Kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya kazi katika Benki Kuu ya Tanzania kama mchumi. Ninakwenda Wizara ya Fedha kusimamia mambo manne ambayo ni uadilifu, ushirikiano, jitihada na huduma madhubuti ambazo zitatolewa kwa wakati mwafaka.
- Alfred Real MC · Top in hood at Hot Three Tenants CompanyUtu wema na busara ya kiongozi aliye bora haijengwi kwa elimu aliyonayo na ama skendo za kujengewa chuki na tuhuma ndan yake. Bali huja kutokana na ni mazingira gani kiongozi anaweza kuwa mbali na mambo yake binafsi kupitia nafasi yako na kufanya kazi kwa ajili ya maslahi ya watu wako.
- Sakina Chamshama · Follow · Top Commenter · PERSONAL SECRETARY II at Tanzania Export Processing Zone Authority - EPZAelimu yako sio mbaya lakini tumia madaraka uliyopewa kwa faida ya watanzania wote, hongera
- Phocus Mbunda · University of Dar es SalaamChapa kazi,mshirikishe Mungu katika utendaji wako,Mungu atakusaidia.
- Saidi Mzingi · Works at Barclays Bank TanzaniaAmejitahidi Kupenyapenya sasa atavaa yale makofia yake
- Nevvy Mdee · Follow · Top Commenter · Arusha, TanzaniaSIo mbaya ila cha muhimu tumia maneno malaini kwa wananchi.
Related posts
Share this post
0 comments: