RAIS UHURU KENYATTA AKATA MITAA PASIPO WALINZI
Posted in
No comments
Tuesday, February 11, 2014 By Unknown
Hii imetokea kwenye mji mkuu ambao ni Nairobi pale Rais Uhuru Kenyatta alipotumia gari moja tu bila msafara akitokea Ikulu kwenda kwenye hoteli moja kwa ajili ya kukutana na Wanafamilia.
Unaambiwa toka amechukua madaraka, Rais Uhuru amekua na tabia hii mara kwa mara tofauti na Rais Kibaki ambae kila sehemu aliyotia mguu ni lazima aambatane na msafara hata kama ni maeneo ya karibu na Ikulu.
Askari mmoja wa usalama barabarani alipigwa butwaa pale alipojikuta kasimamisha gari ambalo ndani yupo Rais Uhuru bila msafara ambapo President mwenyewe alimwambia >>> “Ni mimi ofisa, fungua”. akimaanisha ni yeye amfungulie njia aendelee na safari.
Askari wa Usalama barabarani nchini Kenya wanasifia uongozi wa Rais Uhuru kwamba hata kukiwa na msafara huwa hawawekwi barabarani kwa muda mrefu kuusubiria upite manake wakati wa Mwai Kibaki ilikua inawalazimu wakae barabarani kwa saa kadhaa kabla ya msafara kupita.
Related posts
Share this post
0 comments: