GARI YA BABU AYUBU NA NYUMBA YAKE KUHARIBIWA NA MVUA
Posted in
No comments
Tuesday, April 1, 2014 By Unknown
Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa 28 March 2014 imeleta maafa maeneo Kimara na Kuvunja Nyumba ya msanii wa Sauti na Muziki wa Kizazi Kipya maarufu kama Babu Ayubu, yeye mwenyewe anasema siku hiyo alirudi saa saba usiku na kujifungia ndani kwake lakini ilipofika mida ya saa kumi usiku akaskia kishindo.
Na alipoinuka kutoka kitandani akaona maji yapo kimo cha ugoko wake akajaribu kufungua mlango ukawa haufunguki kumbe ukuta ulikua umeangukia mlangoni na kuzuia usifunguke ndipo alipopiga makelele kwa majirani, wakafika na kumpa msaada lakini alipotoka nje akakuta gari lake limepondwa na matofali 1200.
Babu anasema Gari hilo haliwezi tena kukaa barabarani so itabidi auze kwenye vyuma chakavu na kuhusu kulala amesema atalala katika nyumba yake nyingine kwasababu alikua amejenga nyumba tatu katika eneo moja na iliyoathirika ni moja tu.
See more at: http://www.makorokocho.co/2014/03/you-heard-mvua-yavunja-nyumba-na-gari.html#sthash.fNDXNdIU.dpuf
Related posts
Share this post
0 comments: