JUMA NATURE ADAI KUIBIWA WAZO LA KUANZISHA MRADI WA NDALA NA JOKATE
Posted in
No comments
Saturday, April 12, 2014 By Unknown
Chelewa chelewa, utakuta mwana sio wako!! Ndicho kilichotokea kwa Juma Nature ambaye wazo lake la kuanzisha ndala liliendelea kuwa la mdomoni na ‘kutalk the talk’ hali Jokate Mwegelo akileta action kweli kwa ‘kuwalk the walk’. Baada ya mwanamitindo na mtangazaji Jokate Mwegelo kuanzisha ndala zake kupitia brand yake ya Kidoti, Juma Nature ambaye nae alikuwa na wazo hilo kwa muda mrefu, amefunguka na kusema Jokate amemgeza.
Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM leo,Juma Nature amesema kuwa ingawa Jokate ametoa tayari ndala zake, naye pia ataingiza sokoni brand yake.
“Nani katoa we?”, alihoji Juma Nature aliyeonekana kutokuwa na habari hiyo. “Najua ni msanii mwenzangu lakini inakuwaje! kama ametoa itakuwa ameiga nanihii yangu mimi fresh tu,mwache zimsaidie maisha, si idea yangu hiyo! Kutoa ni lazima nitoe kwasababu mimi naitwa Nature,Nature ni yule yule wa miaka na miaka,hatopotea hata kidogo. Mimi bado kidogo kwasababu na mambo mengi sasa hivi nafanya katikati hapa nadhani mashabiki wangu wakitaka kujua waangalie katika TV. Nadhani kila mtu anajua kwasababu gani? Hakuna msanii ambaye alishawahi kutangaza kwamba anategengeneza project ya ndala zaidi yangu.”
Related posts
Share this post
0 comments: