MOJA KATI YA VIDEO AMBAZO ZIKO MBIONI KUFUNGIWA KUTOKA NCHINI KENYA.
Posted in
No comments
Wednesday, June 11, 2014 By Unknown
Wiki kadhaa zilizopita, Kundi la muziki la Sauti Sol la Kenya liliachia video yake ya Nishike ambayo baadae ilifungiwa kuchezwa kwenye vituo vya Televisheni kutokana na madai ya kutokuwa na maadili, Lakini sasa nae mwanadada Sanaipei Tande ameachia Video ya wimbo wake unaotamba kwenye vituo mbalimbali vya Radio Kenya “Mfalme Wa Mapenzi” ambapo tayari mitandao imeanza kuandika kuhusiana na video na kusema iko mbioni kufungiwa kutokana na maudhui yake.
Video hiyo inaonyesha Scene mbalimbali za kimapenzi imeonekana kuwashtuka watu wengi na kuwa gumzo kwenye mitandao ambapo tangu kuachiwa kwake jana tu tayari imeangaliwa zaidi ya mara 16,000 katika mtandao wa Youtube, swali ni Je itafanikiwa kuchezwa katika vituo vya Televisheni nchini humo?
Itazame Video yenyewe hii hapa.
Related posts
Share this post
0 comments: