MASTAA WAMFUNGUKIA WEMA BILA KUMFICHA KITU
Posted in
No comments
Thursday, January 30, 2014 By Unknown
Stori: HAMIDA HASSAN NA GLADNESS MALLYA
MASTAA wa kike Bongo wamecharuka na kutoa yao ya moyoni baada ya nyota mwenzao, Wema Sepetu kubwagwa na aliyekuwa mpenzi wake, anayetambulika kwa jina moja la Clement na kumnyang’anya vitu alivyompa kama zawadi wakati wa mapenzi yao.
Kuhusu Wema kuporwa ofisi yake ya Endless Fame Film Production, kupewa notisi ya nyumba aliyokuwa amepangiwa na kigogo huyo anayeelezwa yupo serikalini na kunyang’anywa magari siyo stori kabisa mjini.
Risasi Mchanganyiko lilifanya mahojiano na mastaa hao wikiendi iliyopita, kwa njia ya simu na kuwahoji kuhusu kitendo alichofanyiwa mwenzao ambapo walifunguka bila wasiwasi wowote.
USENGENYAJI
Wakali hao, waliopata kuzungumza na waandishi wetu kwa nyakati tofauti, baadhi wamemponda Wema kwa kutokuwa makini wakati akiwa kwenye uhusiano na kigogo huyo kwa kutaka kukabidhiwa hati za vitu alivyopewa.
Wa kwanza kuzungumza ni Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye alisema: “Mimi namshukuru Mungu kwa sababu sijapangiwa nyumba na mwanaume. Naishi maisha yangu simpo ya furaha na amani, sipendi kuigiza maisha. Hao wasanii wanaopenda mambo makubwa wakati hawana uwezo, nawashauri wafanye kazi, filamu zinalipa sana. Wasipende vitu vya haraka, maana siku zote vizuri huja taratibu.”
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
“Mastaa tusijiachie sana kwa wanaume, kama ukipewa gari, upewe na kadi... tusidanganyike na tusipende kuhongwa, tutafute vya kwetu. Kama mtu anakupenda na anakusaidia kwa mapenzi mema, sawa mheshimu.”
WASTARA JUMA
“Inabidi tujitambue jamani, maana kuna watu wanatembea na mastaa makusudi ili wajulikane au kwa manufaa yao wenyewe. Tuache kuishi kwa kutegemea migongo ya wengine. Wengi hawana mapenzi ya kweli. Hata kama mmeachana, sasa kuna sababu gani ya kumnyang’anya mtu vitu ulivyompa?”
NURU NASSOR ‘NORA’
“Mimi najisikia vibaya sana... kama mtu unajiamini una kipaji, kwa nini usifanye kazi? Mastaa tuache kujitangaza, kwa sababu tunatumika kama vyombo vya starehe tu. Tutafute ndoa, tusitumie ustaa kufanya ufuska kwa sababu mali zinapita na mwisho wa siku tunaharibu maisha yetu.”
TAMRINA POSH ‘AMANDA’
“Utapeli ni mwingi, haya mambo ya kupewa vitu siyo vizuri kabisa, tuache. Wanawake tuna akili fupi sana na tunajisahau tunapokuwa na wanaume wakati wenyewe wana kitu moyoni mwao, akishapata anachotaka anaanza matatizo.
“Bora nitembelee taksi au Bajaj kuliko kudhalilishwa... wanawake ni wajinga na huwa tunajidanganya kwa vitu visivyo vyetu, mwisho wa siku tunaumbuka. Tuache sifa za kijinga.”
HABARI: GLOBAL PUBLISHERS
Related posts
Share this post
0 comments: