MTOTO ALIYEDAIWA KUFUFUKA AZUNGUMZA YALIYOMSIBU HUKO GEITA
Posted in
No comments
Wednesday, January 1, 2014 By Unknown
Maulidi alitoweka ghafla Januari 1, 2011. Wazazi wake wanasema siku hiyo aliondoka nyumbani asubuhi na kupeleka mbuzi malishoni, na kwamba siku hiyo hakurudi, jambo lililowatia mashaka wazazi wake hivyo kuamua kutoa taarifa polisi na kwa uongozi wa kijiji.PICHA|MAKTABA
KWA UFUPI
Hali hiyo iliwalazimisha wazazi wake kushirikiana na Jeshi la Polisi kumpeleka Haospitali ya Wilaya ya Geita ili apatiwe matibabu, lakini ni kama hawakuona mtoto wao akipata nafuu hivyo waliondoka naye na kuamua kumpeleka Kigoma Kambako anapatiwa tiba za jadi.
Ni hivi karibuni, Mji wa Geita na maeneo jirani ulikubwa na taharuki ya aina yake,pale mtoto Shabani Maulid (15) anaedaiwa kwamba alifariki dunia miaka mitatu iliyopita, alipoonekana akiwa hai katika Kijiji cha 14 Kambarage, Mtaa wa Mbugani.
Tukio hilo lilizua hofu kwa wakazi wa Mji wa Geita huku waliowengi wakitaka kujua mtoto huyo aliyekutwa amefariki dunia baada ya kupotea kwa siku nne mwaka 2011 na mwili wake kuzikwa, inakuwaje leo hii anaonekana akiwa hai?
Tukio hilo lililotokea Septemba mwaka huu linashuhudiwa na wazazi wa Shaban, ndugu zake, jamaa na hata majirani wa eneo hilo ambao pia wanahoji, je aliyezikwa wakati mwili wa mtoto huyo ulipookotwa ni nani na je mwili wake uko kaburini au la?
Maswali haya na mengine, yalikosa majibu kwani baada ya kuonekana kwake, Shaban hakuweza kuongea vizuri na alionekana kutofahamu kabisa Kiswahili, lugha ambayo kabla ya kutoweka kwake aliifahamu vyema. Wakati huu mtoto huyu anaongea Kiha, japo nayo kwa tabu.
Hali hiyo iliwalazimisha wazazi wake kushirikiana na Jeshi la Polisi kumpeleka Haospitali ya Wilaya ya Geita ili apatiwe matibabu, lakini ni kama hawakuona mtoto wao akipata nafuu hivyo waliondoka naye na kuamua kumpeleka Kigoma Kambako anapatiwa tiba za jadi.
“Niliamua nimpeleke kwa waganga wa jadi huku nyumbani Kigoma na sasa hali inaendelea vizuri kwani anaweza kuongea japo ni kwa muda mfupi kisha hunyamaza”, alisema baba mzazi wa mtoto huyo, Maulidi.
Shaban alikuwa wapi?
Shaban hivi sasa anaendelea vizuri na ‘tiba’ anayopata huko Kigoma na aliweza kuzungumza na gazeti hili kwa simu, huku akieleza kutoweka kwake, pia huko alikokuwa kwa miaka mitatu, huku akiweka bayana kwamba hivi sasa anawatambua vizuri
wazazi na ndugu zake.
Alisema anakumbuka Januari 1, 2011 aliondoka nyumbani kwao na kuelekea malishoni kuchunga mbuzi, na wakati akiwa machungani ghafla lilitokea kundi la watu ambalo lilimzunguka.
Shabani anasema katika kundi hilo alikuwamo mwanamke ambaye hakumtaja kwa maelezo kwamba anashindwa kutamka jina lake, ambaye alimshika mkono na kumtaka waondoke eneo hilo.
Habari: Mwananchi
Related posts
Share this post
0 comments: