MUME WA AUNT EZEKIEL ASHIKILIWA NA POLISI HUKO DUBAI
Posted in
No comments
Thursday, January 2, 2014 By Unknown
Na Hamida Hassan
STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amekiri mumewe kukamatwa na kupata misukosuko lakini si kufungwa kama baadhi ya watu wanavyoeneza uzushi.
Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunt alisema mumewe, Sunday Demonte alikamatwa kutokana na viza yake kuisha ambapo alishikiliwa kwa muda na alipokamilisha taratibu za ‘kurinyuu’, aliachiwa.
“Nashangaa sana mambo haya yamevuma kuwa mimi nimemuacha mume wangu amefungwa, ukweli ni kwamba mume wangu yuko huru na hata sasa ukitaka ongea naye, ni mwanamke gani atakuwa na furaha hivi wakati mumewe ana matatizo?” alihoji Aunt.
Katika mistari mingine, Aunt alisema watu wengi wanatamani kuona ameachika au kujua mwenendo wa maisha yake na mumewe lakini wanajidanganya kwani yeye ni mwanamke aliyeamua kuolewa na amefundwa hivyo wataambulia patupu.
“Siyo rahisi mimi kutoa siri ya maisha ninayoishi na mume wangu, ni makubaliano yetu. Kimsingi ndoa yetu iko imara, watasubiri sana na watachoka wenyewe,” alisema Aunt.
Related posts
Share this post
0 comments: