SERIKALI YAFUNGUKA JUU YA KIFO CHA WILLIAM MGIMWA
Posted in
No comments
Thursday, January 2, 2014 By Unknown
Rais Jakaya Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri huyu wa fedha William Mgimwa na kwamba taifa limempoteza katika kipindi ambacho linamuhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa.
Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue ambae ndio ametangaza kifo cha Waziri huyu kwa niaba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, amesema Mgimwa amefariki saa tano na dakika 20 asubuhi hospitalini Afrika Kusini.
Maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa Marehemu yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia na kwamba taarifa zaidi zitazidi kutolewa kadri zitakavyopatikana.
Related posts
Share this post
0 comments: