SNURA AKIMBIA DENI LA PRODUCER WAKE
Posted in
No comments
Wednesday, January 22, 2014 By Unknown
Stori: Shani Ramadhani na Mayasa Mariwata.
STAA wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi ameingia kwenye majanga baada ya kudaiwa kukacha na deni la prodyuza Mohammed Kandoro wa Studio za Fire Music ambaye alimrekodia nyimbo kadhaa wakati akisaka kutoka.
Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika zinasema kuwa Snura ameingia mitini na kiasi cha Tsh. 400,000 za prodyuza huyo na kwamba sasa amehamia studio nyingine.
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Kandoro na kumwuliza kuhusu ukweli wa minong’ono hiyo, ambapo alikiri na kusema: “Ni kweli namdai laki nne. Nimefanya naye kazi kwa muda mrefu lakini sasa naona ameamua kuondoka na deni langu.”
Snura alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu madai hayo, alifunguka: “Kama kuna deni basi meneja wangu HK (Hyper Man) ndiye anayehusika, maana kila kitu nilimkabidhi yeye na naamini alilipa, sasa kama hakulipa hayo ni mambo yanayomhusu yeye, si mimi tena.”
Katika kutafuta mzani wa habari, gazeti hili liliwasiliana na meneja wa Snura, HK ambaye alisema hana deni lolote analodaiwa na Kandoro, ingawa alikiri kumhamisha Snura studio.
“Kilichopo ni kwamba tumehama kwenye hiyo studio, sina ugomvi nao wala Snura hajawahi kutofautiana naye. Tumefanya hivi kwa lengo la kutafuta ladha tofauti... hayo mambo ya madeni, si kweli.
Hivi kama leo hii tunaweza kulipa zaidi ya shilingi milioni moja na laki nne (1,400,000) tunashindwaje kulipa laki nne tu? Hayo ni maajabu,” alisema HK.
Source: GPL
Related posts
Share this post
0 comments: