WANAFUNZI 13 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI HUKO SINGIDA
Posted in
No comments
Monday, January 20, 2014 By Unknown
Hali ilivyokuwa baada ya ajali hiyo.
Habari zilizotufikia sasa hivi kutoka Singida zinasema watu 13 wamefariki dunia baada ya kutokea ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Isuna mkoani humo.
Habari zinasema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Noah na lori ambayo namba zake za usajili hazikupatikana mara moja. Watu 13 waliofariki walikuwa katika Noah iliyokuwa ikitokea Itigi na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida.
Baada ya ajali hiyo, dereva wa lori na msaidizi wake walitokomea kusikojulikana.
-GPL
Related posts
Share this post
0 comments: