BAADA YA DAVID MOYES KUONDOKA, HATIMAYE HISA KUONGEZEKA MANCHESTER UNITED.
Posted in
No comments
Wednesday, April 23, 2014 By Unknown
Wakati kocha Sir Alex Ferguson alipostaafu kama meneja wa Manchester United mwezi wa tano mwaka jana, hisa za klabu hiyo kwenye soko la hisa la New York thamani yake ilishuka kutoka kuuzwa $18.44 mpaka $15.16 ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tu!
Chini ya utawala wa David Moyes thamani yake iliendelea kushika kwa kasi, mpaka kufikia wiki ya 52 ya utawala wa Moyes thamani ya hisa hizo ilifikia $14.26 kwa hisa moja.
Lakini tangu mwishoni mwa mwezi tano, wakati tetesi za kutimuliwa kwa David Moyes zilipoanza kusambaa thamani ya hisa hizo ikaanza kupanda, na jana tu baada ya kuthibitishwa kwa taarifa kwamba Moyes kibarua kimeota nyasi, thamani ya hisa za Man United ikapanda kwa kasi.
Mpaka kufikia jana jioni thamani ya hisa za MUFC ilikuwa ni $18.78 kwa hisa moja.
Related posts
Share this post
0 comments: