BWENI LA WANAFUNZI KATIKA SHULE YA IVUMWE MKOANI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO.
Posted in
No comments
Wednesday, April 23, 2014 By Unknown
Mbeya:
Bweni la wanafunzi katika shule ya Jumuiya ya wazazi ya Ivumwe inayopatikana jijini Mbeya inayomilikiwa na Chama cha Mapinduzi, limeungua moto jana asubuhi majira ya saa tatu.
Ingawa mpaka hatua hii haijajulikana nini hasa chanzo cha moto huo
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo ndugu Victory Kanama, amekieleza chanzo
chetu kuwa moto huo uligunduliwa na wananchi waliokuwa wakipita eneo la
bweni hilo la wanafunzi wa kiume wakati huo wanafunzi wakiwa darasani
wakiendelea na masomo.
Pamoja na hayo, inasemekana kuwa mali za wanafunzi zimeteketea na moto katika moto huo ikiwemo vitanda, magodoro.
Mwenyekiti huyo wa bodi ya shule ya Ivumwe ametaarifu kuwa hakuna mwanafunzi yeyote aliyepoteza maisha isipokuwa mwanafunzi mmoja ambaye inasemekana alipata jeraha mkononi na kitu kinachosadikika kuwa ni kioo katika harakati za uokoaji.
Habari: Chanzo chetu
Related posts
Share this post
0 comments: