Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

KAJALA AOMBA NAFASI YA KUSIKILIZWA NA WEMA

Posted in
No comments
Wednesday, April 9, 2014 By Unknown

Nimefuatilia kwa karibu ugomvi unaoendelea kati yenu, moyoni imeniuma na nimeona naweza kuwashauri mawili matatu, nanyi mkiona inafaa, muyachukue kama dira ya tatizo lililopo kati yenu.

Kwanza kabisa, kiini cha ugomvi wenyewe mpaka sasa ni kama hakina mashiko. Ugomvi unaendeshwa kwa maneno maneno zaidi ya uhalisia. Nilisikia eti, sababu ya ugomvi wenu ni hii; mlikutana saluni Masaki, Kajala akiwa amelowana kwa jasho kwa vile alitokea mazoezini, Wema alipotaka kumkumbatia, Kajala akakataa kwa nia nzuri ya kutomchafua mwenzake – hapo bifu likaanza.

Inawezekana wakati Kajala akifanya hivyo, alikuwa na nia njema tu, lakini Wema akahisi labda mwenzake anajisikia! Ni kawaida, hatuwezi kufanana mioyo na mawazo.

Tatizo ni pale wanapotokea watu wengine ambao wanakuza huo ugomvi. Kuna watu wanajiita Team Wema, hao nadhani hawana kazi. Wanakesha kwenye mitandao ya kijamii kuchochea huo ugomvi.

Mara inasemwa sijui mmenyang’anyana bwana, mara mmepigana na mengine mengi. Ya nini yote hayo? Kuna wakati hao Team Wema walianza kusema Kajala anatakiwa kurudisha milioni 13 za Wema ambazo alilipa faini mahakamani.
Jamani, thamani ya milioni 13 kwenye matatizo inafanana na kiasi kama hicho kwenye furaha? Siamini kama Wema anazitaka hizo fedha. Alizitoa kwa moyo kwa lengo la kumsaidia rafiki yake.



Niliona picha zilizopigwa mahakamani, wote mlikuwa mnamwagika machozi. Naamini hayakuwa ya kinafiki – ilikuwa furaha. Kwa nini leo mtofautiane kwa jambo dogo? Hata kama ni kubwa, maana inawezekana mna kitu kingine mnachogombania ambacho sikijui, lakini bado nasema kuna kila sababu ya kumaliza hizi tofauti.

Amini msiamini, tofauti zenu hazina maana yoyote. Mtashindwa kufanya mambo makubwa ya maana kwa faida yenu na kubaki mnaendekeza ugomvi ambao mnaweza kuuepuka.

Ninyi ni binadamu, najua mna mioyo, najua kila mmoja anaamini katika imani yake. Uadui umekatazwa kwenye vitabu vyote vitakatifu. Visasi vimezuiwa kabisa kwenye vitabu vyote. Hekima na busara ni sifa njema.

Kusameheana ni kitu kinachoonesha uungwana wa hali ya juu kwa binadamu mkamilifu. Bado mnayo nafasi ya kuzungumza. Hakika nawaambia, mnapoteza mambo mengi ya maana kwa kuendekeza hilo bifu.

Hebu tulieni, vuteni picha wakati Wema unamsaidia mwenzako pale mahakamani, ilikuwaje? Siamini kama ulikuwa unajionyesha kuwa unazo! Sitaki kuamini kuwa una pesa za kuchezea. Bila shaka ulikuwa ni msaada wako kwa kuguswa na matatizo ya mwenzako.

Asitokee mtu akatumia kigezo hicho kuwagombanisha. Huu ugomvi unaweza kuwa na faida kwa watu wengine, siyo ninyi. Mlaanini shetani.
Nawapenda sana dada zangu. Ni furaha yangu kuwaona pamoja tena mkili songesha kwenye tasnia yenu. Ni wakati wenu wa kutafakari! Inawezekana.
Yuleyule,
Mkweli daima,

Habari: Joseph Shaluwa

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.