KUNA WANAWAKE WANAOTOA RUSHWA YA NGONO KUPATA TAJI LA MISS TANZANIA
Posted in
No comments
Wednesday, April 30, 2014 By Unknown
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, ambao ni waandaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga amedai kuwa wasichana wengi wanaoingia kwenye mashindano ya Miss Tanzania hufanya mbinu za kuwalaghai baadhi ya watu kwenye kamati kwa kuwapa rushwa ya ngono ili washinde taji la miss Tanzania.
Akizungumza na Global TV, Lundenga amedai kuwa kuna wasichana wanaoingia kwenye mashindano hayo wakiwa tayari kwa kila kitu.
“Kikumbwa ninachokwambia kuna wasichana ndani ya wasichana,kuna wasichana mule ambao katika mashindano yanayokuja they are ready for every thing,wapo wasichana hao na sisi tunajua hivyo,wasichana wanakuja pale wameshajua mimi nimegombana na boyfriend wangu nimemuacha boyfriend wangu kanikataza,mama yangu, baba yangu nimekuja kwajili hiyo, nilazima nishinde, sasa anashindaje? Lazima apitepite kwa viongozi sisi,wanapitapita sana,wanajilegeza sana kwetu sisi,sasa sisi kama hatuna ethics ndiyo tunaingia kwenye mtego mbaya,kwasababu kuna mtu kwenye kamati yetu tumeshamsuspend mara mbili,tunamsuspend kwasababu ya upumbavu wake, mara mbili tumeshamsimamisha kwasababu ya upumbavu wake,” alisema.
Kuhusu tuhuma za kuwauza warembo watu wenye pesa, Lundenga alisema: Unajua hapa mjini, mimi leo siwezi kusema Musofe simjui,siwezi sema mapedejee gani simjui, najuananao ndio watu wa mjini hao,tunakula nao tunalala nao, si ndio! Sasa huwezi sema completely ukaknock-out, haiwezekani,no it’s very difficult, akina nani wote wa Musoma yule,akina nani, huwezi, hao ndio mapedejee wa mjini.”
Related posts
Share this post
0 comments: