MUME WA FLORA MBASHA ASAKWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI.
Posted in
No comments
Thursday, May 29, 2014 By Unknown
JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.
Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi Na. TBT/IR/1865/2014 akidai kufanyiwa unyama huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili) wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar.
Ilidaiwa kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili ilidaiwa alitekeleza ukatili wake huo ndani ya gari lake hali ambayo ilimfanya mlalamikaji kutoa taarifa Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar.
Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu makali aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi aende Hospitali ya Amana na kugundulika kuwa aliingiliwa kimapenzi na kumsababishia michubuko sehemu za siri.
HISTORIA YA MLALAMIKAJI
Mlalamikaji ni kati ya watoto mapacha waliozaliwa jijini Mwanza na mama ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Mama wa mtoto huyo (kwa sasa ni marehemu pamoja na mume wake) akiwa muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God (EAGT) aliamua kumtoa mtoto mmoja kwa mama mzazi wa Flora Mbasha kwa lengo la kumlea, wakati huo mtoto huyo alikuwa na miezi mitatu.
Ikaelezwa kuwa, mama wa Flora alikaa na mtoto huyo akimsomesha hadi alipofika darasa la saba ambapo alimkabidhi kwa Flora na kuishi naye hadi alipofikwa na janga hilo.
Maelezo zaidi yanasema Mbasha aliweza kufanya kitendo hicho kwa sababu mkewe (Flora) ameondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini kwa kile kilichodaiwa kwamba kuna ugomvi mkubwa ndani ya ndoa yao.
Taarifa zaidi zinadai kwa sasa Mbasha naye hayupo nyumbani kwake huku mlalamikaji yuko Hospitali ya Amana akiendelea kufanyiwa uchunguzi wa kiafya ili kubaini kama ana maambukizi ya magonjwa ya zinaa au la!
Kwa upande wake mlalamikaji huyo alipopigiwa simu juzi kwa lengo la kuthibitisha kuhusiana na sakata hilo alikiri na kusema amekwishatoa taarifa polisi kwa kitendo alichofanyiwa na mwenye nyumba huyo huyo.
Related posts
Share this post
0 comments: