SOMA HAPA KUHUSU WANAWAKE WALIOBAKWA NA KUNING'INIZWA MTINI HUKO NCHINI INDIA.
Posted in
No comments
Friday, May 30, 2014 By Unknown
Takribani
wanaume watatu akiwemo afisa mmoja wa polisi tayari wamekamatwa
kuhusiana na tukio la kubakwa kwa wasichana wawili wadogo na kundi la
watu na kuning’inizwa juu ya mti huko nchini India.
Mamlaka katika Jimbo la Utter Pradesh limesema kuwa bado linamsaka
mtu mmoja ambaye anatuhumiwa kuwepo katika kundi hilo lililohusika
kufanya tukio hilo la kusikitisha.
Familia za wahanga wa tukio hilo zimesema kuwa mara ya kwanza polisi
walikataa kuwasaidia katika kuwatafuta watoto hao baada ya kupotea
ambapo matukio ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake nchini India
bado yameendelea kuwa tatizo kubwa.
Wanakijiji walikuta miili ya wasichaa hao wenye umri wa miaka 14 na
15 ikiwa inaning’inia juu ya mti wa maembe saa chache baada ya kupotea
nyumbani katika kijiji cha Katra kilichopo kwenye jimbo la Utter
Pradesh.
Wasichana hao walikuwa wamekwenda vichakani kuoga kutokana na
kutokuwa na vyoo nyumbani kwao ambapo mamia ya wanakijiji wenye hasira
walikusanyika katika eneo hilo la mti kwa siku nzima wakiandamana
kushinikiza polisi kukabiliana na vitendo hivyo.
Related posts
Share this post
0 comments: