WAPINZANI BUNGENI WAMKAANGA ZITTO KABWE
Posted in
No comments
Friday, May 30, 2014 By Unknown
Dodoma.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana ilimlipua mbunge kutoka kambi yao, Zitto Kabwe ikimhusisha na ufisadi wa Sh119 milioni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana ilimlipua mbunge kutoka kambi yao, Zitto Kabwe ikimhusisha na ufisadi wa Sh119 milioni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).
Hii ni mara ya kwanza kwa kambi ya upinzani
kumhusiaha mbunge ‘mwenzao’ na tuhuma za ufisadi tofauti na kawaida yao
ya ‘kuwashughulikia’ ubadhirifu katika Serikali.
Zitto, mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya
Chadema na ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), anadaiwa kuchota fedha hizo kupitia kampuni ya Leka
Dutigite ambayo ina hisa nyingi katika kampuni nyingine ya Gombe
Advisors Limited ambayo Zitto ni mkurugenzi wake.
Akiwasilisha maoni ya upinzani bungeni jana kuhusu
makadirio na matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
mwaka 2014/15, waziri kivuli wa wizara hiyo, Joseph Mbilinyi alisema
Zitto hakutakiwa kuchota fedha hizo kwa kuwa anabanwa na sheria ya
maadili ya viongozi wa umma.
Alisema Zitto, ambaye katika miezi ya karibuni
aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa chama chake, ni mwenyekiti wa PAC,
kamati ambayo jukumu lake ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu
ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika wizara na mashirika ya umma,
yakiwamo Tanapa na NSSF, hivyo kulikuwa na mgongano wa kimasilahi katika
suala hilo.
Tuhuma za Zitto
Katika hotuba yake, Mbilinyi alisema taarifa za
kibenki ambazo kambi hiyo imezipata zinaonyesha kuwa Desemba 10, 2012,
Hifadhi ya Taifa ya Saadani ilihamisha Sh12 milioni kwenda katika
akaunti ya kampuni ya Leka Dutigite.
“Siku moja baadaye fedha hizo zilitolewa kwa pesa
taslimu kutoka kwenye akaunti hiyo. Januari 14 na Februari 7, 2013
akaunti ya Leka Dutigite iliingiziwa Sh28.6 milioni,” alisema Mbilinyi.
Sugu alisema fedha hizo ziliingizwa na mtu aitwaye Mchange na kwamba ilipofika Februari 7 zote zilikuwa zimetolewa.
Alisema Februari 28 mwaka jana, akaunti ya Leka
Dutigite iliingiziwa Sh32.3 milioni kutoka NSSF na kwamba siku hiyo hiyo
fedha hizo zilitolewa kwenye akaunti hiyo. Siku nne baadaye shirika
hilo lilifanya malipo mengine kwenye akaunti ya Leka Dutigite.
“Ziliingizwa Sh46.6 milioni ambazo zilitolewa
kutoka kwenye akaunti hiyo kwa mikupuo miwili. Katika kipindi cha miezi
mitatu, kati ya Desemba 10, 2012 na Machi 4, 2013 kampuni hiyo (ya
Zitto) ililipwa Sh119.9 milioni kwa utaratibu huohuo wa ingiza-toa
fasta,” alisema Mbilinyi.
Alisema kati ya fedha hizo Sh12.2 milioni zililipwa na Tanapa na Sh79 milioni zililipwa na NSSF.
Habari: Mwananchinewspaper
Habari: Mwananchinewspaper
Related posts
Share this post
0 comments: