HII NDIYO MELI YA JAPAN ILIYOLIPUKA BANDARINI.
Posted in
No comments
Friday, May 30, 2014 By Unknown
Mlipuko
mkubwa umetokea kwenye meli kubwa ya mafuta nchini Japan katika Pwani
ya Kusini Magharibi mwa bandari ya Himeji na kusababisha mtu mmoja kati
ya wanane waliokuwa ndani ya meli hiyo kupotea huku wengine wanne
wakijeruhiwa vibaya.
Moto mkubwa ulilipuka katikati ya bahari ambapo meli hiyo yenye uzito
wa tani 998 iliyokuwa ikitokea mji wa Hiroshima kuachwa ikielea ndani
ya maji baada ya ajali hiyo na baadae kufatwa na meli za kupambana na
majanga ya moto.
Watu saba wameokolewa katika ajali hiyo mbaya, wanne wakiuguza
majeraha ya moto kwa mujibu wa shirika la habari la NHK, ambapo kapteni
wa meli hiyo amesema uchunguzi kumtafuta mtu mmoja aliyepotea bado
unaendelea.
Afisa usalama katika Pwani hiyo Koji Takarada amesema chanzo cha
mlipuko huo bado hakijajulikana ambapo shirika la habari NHK limeripoti
kuwa wafanyakazi wa meli hiyo walikuwa wakifanya kazi chini ya meli
wakati mlipuko unatoke.
Related posts
Share this post
0 comments: