WANAWAKE 20 WENGINE WATEKWA HUKO NIGERIA.
Posted in
No comments
Tuesday, June 10, 2014 By Unknown
Watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la Boko Haram wamewateka
takribani wanawake 20 karibu na eneo walikowateka wasichana 200 wa shule
Kaskazini mwa Nigeria.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanawake hao waliingizwa ndani
ya magari wakiwa wamenyooshewa mitutu ya bunduki na kupelekwa katika
eneo lisilojulikana katika Jimbo la Borno.
Jeshi la Nigeria ambalo limekuwa likikosolewa kwa kushindwa kuzuia
vitendo vya kigaidi Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo bado halijasema
chochote kuhusiana na tukio hilo.
Licha ya hali ya tahadhari iliyotangazwa katika ukanda huo wakazi wa
eneo hilo wanasema jeshi limekuwa halifanyi chochote au wakati mwingine
kutokuwepo kabisa katika eneo hilo na kuruhusu kundi la Boko Haram
kuendelea kufanya mashambulizi yake.
Kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi kadhaa tangu mwaka 2009
kushinikiza kuanzisha Jimbo litakalofuata sheria za kiislamu nchini
Nigeria ambapo hadi sasa maelfu ya watu wameuwawa katika mashambulizi
hayo.
Tukio la hivi karibuni zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa
katika kijiji cha Chibok karibu na mpaka wa Cameroon April 14 mwaka huu.
Related posts
Share this post
0 comments: