Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

PENZI LA LULU MICHAEL NA AMIR NANDO WA BIG BROTHER LAANIKWA HADHARANI

Posted in
No comments
Tuesday, June 10, 2014 By Unknown


Uhusiano wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa 2013, Amir Nando umewekwa kweupe.
 
Kabla ya wawili hao kufunguka, kulikuwa na madai mazito kuwa Lulu na Nando ‘wanachepuka’ mara tu baada ya Nando kutolewa BBA kwa ukosefu wa nidhamu.
 
Kuna habari kuwa Nando ndiye aliyevujisha ishu hiyo, jambo ambalo Lulu hakupendezwa nalo hivyo kumpiga chini.
 
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa  Wikienda  lilimtafuta Nando ambaye mwanzoni alifanya kama utani akidai Lulu ni mwanamke anayefaa kuolewa (wife material) lakini alipoulizwa kwa msisitizo, alikana kuwa na uhusiano na mrembo huyo.
 
“Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, akikubali freshi nitamuoa. Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake,” alisema Nando.
 
Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyohuyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa.
 
Alifunguka: “Hebu muulizeni Nando kama ni Lulu mimi au mwingine? Yeye akishatoa jibu sina la kusema.”

Habari: Gazeti la Ijumaa/ GPL

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.