Mchekeshaji Tracy Morgan katika hali mbaya baada ya ajali.
Posted in
No comments
Tuesday, June 10, 2014 By Unknown
Mchekeshaji
maarufu wa nchini Marekani Tracy Morgan bado yupo katika hali mbaya
kiafya kutokana na ajali mbaya ya gari aliyopata mwishoni mwa wiki.
Muigizaji huyo wa vichekesho anakabiliwa na majeraha ya kuvunjika
mbavu, pua na mguu baada ya gari aliyokuwa akisafiria kugongwa na gari
kubwa na kusababisha ajali mbaya.
Baada
ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake, Morgan ameanza kuonyesha matumaini
lakini ataendelea kubaki hospitalini kwa wiki kadhaa akipatiwa matibabu,
kwa mujibu wa msemaji wake.
Katika ajali hiyo iliyotokea mjini New Jersey muigizaji mwingine wa vichekesho Jimmy Mack, alipoteza maisha.
Related posts
Share this post
0 comments: