MADEE KUWEKA WAZI KIASI ANACHOLIPWA KATIKA MZIKI.
Posted in
No comments
Tuesday, July 8, 2014 By Unknown
Maisha ya mziki ya wasanii wengi wa Tanzania walio wahi kufanya show nyingi kipindi cha nyuma wanaweza kuwa mashuhuda wa hiki alichokizungumza Madee kupitia Exclusive interview na millardayo.com.
Asilimia kubwa ya wasanii wa bongo fleva kipindi cha nyuma hawakua wakilipwa malipo kama haya ya sasa, miongoni mwa wasanii hao ni Madee ambaye amesema, "Dah kiukweli hela ndogo niliyowahi kulipwa nakumbuka ni 40,000'
‘Hahaha ilikua mwaka 2003/2004 wakati nimetoa wimbo wa kazi yake mola alituita promota mmoja ambaye hivi sasa hivi ni marehemu anaitwa Mnomba,nakumbuka nilienda mimi na babu Tale baadae tukakutana na Dudubaya huko’
‘Tulikuwa tuna enjoy maana hakuna mtu aliyekua anajua kama haya ni maisha show hiyo ilifanyika Triple A,malipo makubwa niliyowahi kulipwa ni mwaka jana 2013 kwenye show za vinywaji baridi nililipwa Milioni 38 kwa show 5′
‘Mkataba aliusaini Babu Tale nikashangaa Babu Tale amekuja akaja katoa hela akasema hela hizi hapa tugawane ni za show zako 5 ilikuwa mwezi wa kwanza nakumbuka"
Madee kwa sasa kaachia wimbo wake mpya unaitwa Ni sheeda ambao umefanyika kwa Marco Chali.
Related posts
Share this post
0 comments: