OLIVER MTUKUDZ MWANAMZIKI MKONGWE, APEWA DEGREE YA HESHIMA YA UDAKTARI.
Posted in
No comments
Tuesday, July 8, 2014 By Unknown
Mwanamziki mkongwe wa kimataifa nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi ametunukiwa tuzo ya tatu iliyobeba heshima ya udaktari kutokana na kuwa mshauri na balozi mzuri wa muziki.
Mwaka 2003 alitunukiwa tuzo kubwa ya heshima na chuo kikuu cha Zimbabwe kwa kutambua miongo kadhaa ya mchango wake na kujitolea katika kujenga muziki na msukumo wasanii wa kizazi kipya nchini Zimbabwe huku akionyesha ushawishi kwenye kazi za wasanii hao.
Mwaka 2009, Chuo Kikuu cha Wanawake cha Afrika kilimpatia tuzo ya shahada ya sanaa na kumwelezea mwanamuziki huyo kama mbunifu wa hali ya juu kuwahi kutoke nchini Zimbabwe katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita.
Oliver Mtukudzi ni mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Zimbabwe ambaye amevuma sana na kuvuka mipaka kutokana na nyimbo zake zinazohamasisha amani na kutoa burudani barani Afrika ambapo amekua akitumika kama alama katika taifa hilo haswa kwa upande wa sanaa ya nchini Zimbabwe.
Related posts
Share this post
0 comments: