WEMA ASHAURIWA AACHE UMAARUFU WA KUBEBWA NA SCANDAL.
Posted in
No comments
Sunday, May 11, 2014 By Unknown
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameibuka na kumuonya Wema Sepetu kupiga kazi na kuepuka umaarufu bila kazi. Nyerere amemtaka Wema aachane na skendo za kila kukicha kwani hazina maana kama kazi ya sanaa aliyoichagua kama njia ya kumuingizia kipato. “Kwanza nampongeza sana Diamond kwa tuzo zote alizopata kwa kuwa alistahili lakini Wema naye anapaswa kuiga mfano, vinginevyo atakuwa maarufu bila ya heshima,” alisema Steve Nyerere.
Related posts
Share this post
0 comments: