HII NDIYO SABABU KWANINI JENIFER ONYESHO LA UFUNGUZI WA MAONYESHO YA KOMBE LA DUNIA HUKO BRAZIL.
Posted in
No comments
Tuesday, June 10, 2014 By Unknown
Michuano ya kombe la Dunia inatarajiwa
kuanza siku ya Alhamisi wiki hii nchini Brazil kwa ufunguzi wa mechi
kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia, lakini kama ilivyo kawaida
kabla ya mechi husika ya ufunguzi kunakuwepo na sherehe za ufunguzi wa
michuano hiyo mikubwa.
Kwa mwaka huu wasanii Jennifer Lopez,
Claudia Leitte na Pitbull walipangwa kutumbuiza lakini kwa mujibu wa
taarifa ambazo tulizipata ni kwamba Jennifer Lopez amegoma kwenda
kutumbuiza katika sherehe hizo za ufunguzi pamoja na kwamba ndio msanii
aliyeimba wimbo rasmi wa michuano hiyo.
Staa huyo ambaye wiki iliyopita aliachana na
mpenzi wake Casper Smart , Jina lake halipo tena katika orodha ya
wasanii watakaosindikiza sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia Alhamisi
hii.
Kwa mujibu wa FIFA, Jennifer Lopez hatofanya
onyesho katika sherehe hizo kutokana na ‘sababu za kiufundi’ ambazo
hazikufafanuliwa ni zipi.
Hata hivyo wasanii wengine walioshirikiana na
JLO kuimba wimbo wa ‘Ole Ole’ – Pitbull na Claudia Leitte ambao wao
watatumbuiza katika sherehe hizo.
Related posts
Share this post
0 comments: