SIGARA KUPIGWA MARUFUKU KUVUTWA MIGAHAWANI, SOKONI NA HOTELINI HUKO URUSI
Posted in
No comments
Monday, June 2, 2014 By Unknown
Ile sheria ya kupambana na uvutaji sigara imeanza kutumika nchini Urusi ambapo sasa ni marufuku kuvuta sigara katika migahawa na maeneo mengine ya kupata huduma za chakula.
Marufuku hiyo pia inatumika katika mahoteli na masoko ikiwa ni pamoja na kwenye vyombo vya usafiri kama treni na meli na katika vituo vya treni za masafa marefu.
Wamiliki wa migahawa na sehemu nyingine za kula wanatakiwa kuondoa vyombo vya kuwekea majivu ya sigara na kubandika matangazo ya onyo la kuvuta sigara kuwatahadharisha wateja kuwa uvutaji wa sigara ni marufuku katika maeneo hayo.
Mmiliki wa kawaida wa maeneo hayo atalazimika kulipa faini ya dola za kimarekani 870 hadi 1150 ikiwa mmoja wa wateja wake atakutwa akivuta sigara. Hii ni pamoja na wamiliki wa biashara kubwa ambao watalipa hela nyingi zaidi kiasi cha dola 1,700 hadi 2,600 kwa kosa kama hilo.
Asilimia 82 ya wamiliki wa migahawa nchini Urusi wanaamini marufuku hiyo ya uvutaji sigara ni unyanyasaji wa moja kwa moja kwa wavutaji na kutarajia idadi kubwa ya wageni kuanzia siku ya kuanza kutumika kwake.
Related posts
Share this post
0 comments: