HIKI NDICHO KIASI KILICHOTUMIKA KUKAMILISHA VIDEO YA WIMBO WA KEREWA WA SHETTAH
Posted in
No comments
Tuesday, July 1, 2014 By Unknown
Muziki wa Tanzania kwa sasa umetoa ajira kwa vijana wengi ambao baadhi yao wameamua kuwekeza kwa hali na mali,katika list ya vijana wanamuziki wa Tanzania ni pamoja na Shettah ambaye singo yake ya Kerewa ameenda kufanyia video yake South Africa.
Kupitia exclusive interview na millardayo.com Shettah amekubali kutaja kiasi kilichotumika ili kuikamilisha video ya Kerewa>>’Video ya Kerewa ukitoa gharama gharama zingine imenigharimu kama Milion 25 za Kitanzania’
‘Yeah Kwa sababu Director God Father peke ake kachukua Milion 19 kuna ndege zile,kukaa,chakula ingawa Dstv pia wameongeza mtonyo lakini kitu kikubwa ni hotel kwa sababu kwa siku tulikua tunalipa pesa za Kitanzania kama 450,000 hivi’
‘Hotel nimeanza kukaa Cape Town nikaenda kukaa Durban baadae Johannesburg yaani hotel pekeake nimetumia zaidi ya Milion 3 za Kitanzania,nina furaha kile nilichoenda kukitafuta nimekipata’.
Via millardayo.com
Related posts
Share this post
0 comments: