KIJANA MMOJA KUTOKA UBUNGO APANDA JUU YA MNARA WA SIMU AKITAKA KUJIUA NA KUTAKA AONGEE NA RAIS
Posted in
No comments
Tuesday, December 31, 2013 By Unknown
Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Hassan kutoka Ubungo Dar es Salaam alipanda juu ya mnara wa simu leo kwa kile alichodai kuwa, anataka kuongea na Rais juu ya unyama aliotendewa na polisi kwa kubambikiwa kesi na kutakiwa kutumikia kifungo cha miaka sita jela. Lakini hakuweza kutimiza adhma yake baada ya kikosi cha zima moto na uokoaji kufanya juhudi kubwa na kufanikiwa kumshusha kutoka katika mnara huo. Alipohojiwa na mwandishi wetu alidai kuwa asingeweza kushuka mpaka aonane na Rais na kumueleza yale yanayomsibu kabla hajajirusha kutoka katika mnara huo na kupoteza maisha kwa kile alichodai kuwa ni uonevu anaotendewa na jeshi la polisi kwa kubambikiziwa kesi asiyohusika nayo.
Pichani ni kijana huyo akiwa juu ya mnara huo na mmoja ya waokoaji akijaribu kufanya juhudi za kutaka kumshusha
Raia Ubungo wakishuhudia tukia hilo la kustaajabisha
Gari ya kikosi cha zima moto na uokoaji likiwasili Ubungo kutoa msaada katika tukio hilo
Askari wa kikosi cha zima moto na uokoaji akishuka na kijana huyo
Kundi kubwa la watu wakishuhudia tukio hilo
Pichani ni kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Hassan baada ya kushushwa kutoka katika mnara huo wa simu
Related posts
Share this post
0 comments: