CCM NA CHADEMA IMEFIKIA HATUA YA KUTUPIANA MAWE. JE, HALI HII ITAISHA LINI NA HATUA GANI ILICHUKULIWA JUU YA WATU HAWA....?
Posted in
No comments
Thursday, January 16, 2014 By Unknown
Hapa tunamuona Mh. Ismail Aden Rage, Mbunge wa jimbo la Tabora mjini kupitia CCM akiwaongoza viongozi mbali mbali wa CCM kumshambulia mpinzani wao wa kisiasa kutoka Chadema kwa silaha yoyote ile iliyo karibu. Kwa hali inavyoonekana pichani sijui ilikuwaje hadi huyu mlengwa akasalimika ila nabaki najiuliza maswali kadhaa...Je kuna hatua yoyote ilichukuliwa dhidi ya hawa hili genge ambalo kwa namna yoyote ile wanaonekana wako tayari hata kuondoa uhai wa mtu.
Je kama washambuliaji wangekuwa viongozi wa Chadema, kweli hadi leo hii wangekuwa bado wanatanua mtaani? Picha kama hizi zinanipa woga kweli kweli huko tunakoelekea...kwamba watu ambao sura zao zinaonekana wazi wazi wakiwa na nia ya kutenda kosa la jinai hawakukamatwa wala kuhojiwa, ni jambo la hatari linaloleta hofu kubwa katika jamii. Nawaomba wote wale wanaoweza kuzitambua hizi sura, tusaidiane kuyataja majina ya hawa watu tuwafahamu na nyadhifa zao ndani ya CCM.
-Jamii Forums
Related posts
Share this post
0 comments: