JUMA NKAMIA AWAANGUKIA WADAU WA HABARI...AOMBA USHIRIKIANO KAULI ZAKE ZAMPONZA
Posted in
No comments
Wednesday, January 22, 2014 By Unknown
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (pichani), amewaomba wadau wa habari kushirikiana naye katika kujenga na kuiboresha tasnia ya habari. Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa ofisi rasmi baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo. “Kwa sasa nimekabidhiwa ofisi ili nipiganie haki na maslahi ya wanahabari na siyo kama watu wanavyofikiria kwamba nimekuja kudidimiza sekta ya habari,” alisema Nkamia.
Aliongeza: “Mimi nimekuwa mwandishi wa muda mrefu na mwanamichezo. Najua changamoto zilizopo katika tasnia ya habari. Kwa hiyo, ndugu zangu waandishi tushirikiane pamoja ili tuweze kutatua matatizo yanayoikabili tasnia hii ya habari kwa jumla.”
Nkamia amekuwa mmoja wa wabunge waliokuwa wakiwabeza wanahabari katika vikao vya Bunge mjini Dodoma.
Miongoni mwa kauli alizowahi kuzitoa zilizoonekana kuwa ni za kukebehi tasnia ya habari, ni ile aliyohoji kama Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri (TEF) ni NGO’s (mashirika yasiyokuwa ya kiserikali) au taasisi ya serikali kiasi cha kutoa tamko na nyingine kuwaita waandishi wengi Watanzania kuwa ni makanjanja.
Related posts
Share this post
0 comments: