HIZI NDIZO SABABU MBILI ZILIZOMFANYA D KNOB KUFUNGA NDOA YA SIRI
Posted in
No comments
Saturday, April 26, 2014 By Unknown
Hit maker wa single mpya ya Nishike mkono D knob leo ame-amplify sababu za kuamua kufunga ndoa ya kimya kimya mwaka 2009 huku idadi ya watu waliohudhuria pamoja na maharusi wenyewe ikiwa sio zaidi ya 10 kuanzia kanisani mpaka walikoelekea baada ya kutoka kanisani.
Ameongea na millardayo.com na kusema ‘nilitaka kuifanya na mwenzangu nikamwambia tumekua wapenzi lakini sasa yahitaji tuwe ndani ya ndoa akasema twenzetu tukaongozana mpaka kanisani padri akasema hamuwezi kuoana nyie mnajua hata ndoa ni nini?kuna hatua’
‘Siyo kitu ambacho tulitaka kufanya kama watu wengi wanavyofanya ile kukaa kuchangishana kwa sababu mimi rafiki zangu wa karibu wote walikua block nisingetaka kufunga ndoa halafu mwisho wa siku tuanze kununiana kuwa huyu hajachanga yule kachanga chapili nilitaka kufanya ili niendelee na maisha yangu kama mtu unapoamua kufanya birthday’
‘Wazazi walipata taarifa mwishoni kwa sababu hata mzee katika risala yake maana tulikaa kwenye meza moja baada ya ndoa mzee akasema mimi sijui nakupa zawadi gani maana umeniambia jana tu,kitu tulichofanikiwa ni gauni la mke wangu maana ni gauni la gharama nashukuru Mungu lilitupa stress mwanzo lakini liliwahi’.
Habari: #millardayo
Related posts
Share this post
0 comments: