Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

IRENE UWOYA: WASANII BADO HAWAJAWEZA KUTHAMINI MUDA.

Posted in
No comments
Wednesday, April 30, 2014 By Unknown


Irene Uwoya 
Na Herieth Makwetta, Mwananchi
Kwa ufupi
  • Akizungumza katika mafunzo maalumu ya wasanii na wafanyakazi wa Kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa filamu 5 Effect, Uwoya alisema kinachokwamisha tasnia ya filamu kufika katika nafasi za juu kimafanikio ni kutokujali muda.

Bagamoyo. Mwigizaji wa filamu na mtangazaji wa kipindi cha redio cha Paradise, Irene Uwoya, amesema licha ya kwamba wasanii wanafanya bidii kuyafikia mafanikio, kikwazo kikubwa katika safari yao ni kutokuthamini muda.

Akizungumza katika mafunzo maalumu ya wasanii na wafanyakazi wa Kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa filamu 5 Effect, Uwoya alisema kinachokwamisha tasnia ya filamu kufika katika nafasi za juu kimafanikio ni kutokujali muda.
“Tatizo kubwa ni kutokuthamini muda, unakuta mmekubaliana kwamba mkutane saa nane mchana katika eneo la kutengenezea filamu (Location), unafika pale mtu unayetakiwa kushirikiana naye katika (Scene) kile kipande hajafika, anafika saa kumi jioni, kazi inachelewa kuanza na muda unapotea,” alisema Uwoya.
Alisisitiza kwamba ikiwa tasnia hiyo itajali muda ipasavyo, inaweza kupiga hatua kubwa kwa mwaka huu, hasa ukizingatia sanaa imerasimishwa na Serikali hivyo ni kazi inayotambulika kwa sasa.
“Serikali yetu imerasimisha sanaa, kwa sasa ni kazi kama ya ofisini, inatakiwa sisi wasanii tulitambue hili na kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anatekeleza majukumu yake ipasavyo.Pia mtu wa kamera naye lazima ajue script (muswada) inasema nini.
Vivyo hivyo kwa upande wa masoko na wasambazaji tunahitaji watu wenye uelewa na elimu kuhusu kazi hizi ili tusonge mbele,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa viongozi ni kama dira, hivyo wanapaswa kutoa mwongozo mzuri kwa wasanii na kusimamia kampuni vema ili kujikwamua na wizi wa kazi za sanaa nchini.
“Lazima tuondoe dhana kuwa bila watu wa jamii ya Asia hakuna usambazaji,” anasema.

Chanzo: Mwananchi.

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.