MR. NICE KUFUNGUKA NAMNA ALIVYOJIKUTA KATIKA MFULIO
Katika hali yakushangaza, Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice,
finaly afunguka kuhusu utajiri wake na sababu za kushuka kwake kimuziki,
katika moja ya interview Mr.Nice alidai kuwa hajui ni nini haswa
kilichotokea ila yote hayo ni mipango tu ya Mungu.Mr.nice alizidi
kufunguka na kusema kuwa, alikuwa na jumla ya zaidi ya shilingi bilioni
1.5 zote zikiwa katika account mbalimbali hapa nchini, na hela zote hizo
zimetoweka katika kipindi cha muda mfupi bila yeye kujua zimetumikaje.
“kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu, kwani sikuwahi
kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu, pesa yote nilikuwa naipata kwa hali,
naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu” alisema
Mr.Nice.
“Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank
tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje
ya nchi kama. Marekani,Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai,
SouthAfrica na kwingineko, na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana”
Alimalizia star huyo kutoka Tzee na mwanzilishi wa staili ya TAKEU.
Mbali na kushuka kwake kimuziki Mr.Nice anakiri kuwa ana-miss sana
enzi hizo kwenye show zake zisizoweza kusahaulika na machozi huwa
yanamtoka kila akumbukapo show aliyopiga nchini Rwanda ambapo hadi
waziri wa nchini humo aliweza kumsubiria airport kumpokea tena kwenye
red carpet huku akisindikizwa na magari ya polisi, pamoja na mashabiki
wake lukuki waliojaza uwanja huo wa ndege kushuhudia ujio wake
Related posts
Share this post
0 comments: