PROFESSOR J ATOA YA MOYONI KWA WALE WOTE AMBAO HAWAKUHUDHURIA MAZISHI YA MUHIDIN GURUMO AKIWEMO DIAMOND
Posted in
No comments
Friday, April 18, 2014 By Unknown
Msanii mkongwe wa Hip Hop, Profesa Jay ameeleza kusikitishwa kwake
kutokana na wasanii wengi wa muziki ya Bongo Flava kushindwa kwenda
kumzika msanii mkongwe wa muziki wa dansi Muhidin Gurumo aliyefariki
Jumapili iliyopita na kudai kuwa wasanii wengi waliishia kuandika tu
R.I.P.
Profesa Jay akiwa kwenye mazishi ya Mzee Gurumo Jumanne hii katika kijiji cha Masaki, Kisarawe mkoani Pwani
Profesa Jay amesema
Profesa Jay akiwa kwenye mazishi ya Mzee Gurumo Jumanne hii katika kijiji cha Masaki, Kisarawe mkoani Pwani
Profesa Jay amesema
“Kiukweli ilinisikitisha sana kwasababu wasanii kule Kisarawe
kiukweli tulikuwa wachache sana,” alisema. “Sikumwona mwingine sijui
hatukuwa karibu karibu, kwasababu labda watu walikuwa wengi lakini
kiukweli niliona wengi wazee ambao nilikutana na akina Abdul Salvado
tukasalimiana, akina Mze Mabela kutasalimiana, akina Ali Choki ndio
niliwaona kule na vitu vingine kama hivyo.
Lakini wasanii wa kizazi
kipya kiukweli hawakuonyesha hivyo vitu. Lakini nimeona wanapost
wanasema, Rest in peace mzee, Rest in peace mzee, lakini physically
hawakuonyesha ushirikiano,iliniumiza kidogo nikasema tupo mjini hapahapa
ofcourse wengine wamebanwa wako nje ya mkoa,walikuwa mbali au wengine
majukumu yaliwabana, lakini sio kiasi hicho tupo wengi sana.
Tungeweza
kuonyesha hivi vitu ni lazima tutokee kwa mfano. Inasikitisha kidogo
labda watu waliona uvivu kuona Kisarawe mbali,lakini Kisarawe ni hapa
tu,” alisema Profesa Jay.
Related posts
Share this post
0 comments: