KISA CHA KAJALA KUWA BALOZI WA WANAWAKE TANZANIA HIKI HAPA
Posted in
No comments
Friday, April 18, 2014 By Unknown
S
Staa maarufu wa filamu hapa Bongo, Kajala Masanja.
Staa
maarufu wa filamu hapa Bongo, Kajala Masanja hivi karibuni alipata
shavu la nguvu baada ya kuibuka kuwa balozi wa wanawake Tanzania nzima
kupitia taasisi ya Women Connect iliyopo jijini Dar.
Akizungumza na mkurugenzi wa taasisi hiyo, Hafsa Semdaiya
alisema wameamua kumchagua Kajala kwa kuamini ni kioo cha jamii na ni
staa wa kwanza kuonesha moyo wa kuitikia wito kwani alianza kwa kutoa
misaada kwenye kituo cha watu walioathirika na madawa ya kulevya.
“Kwa
kweli kigezo kikubwa tulichokiona kwa Kajala ni moyo wake wa kujitoa na
pia tumemuona ni kioo cha jamii na kama mwanamke anayejali, amekuwa
mstari wa mbele kwenye kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye uhitaji,”
alisema Semdaiya.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, taasisi hiyo inajihusisha na vitu vingi ila Kajala atahusika zaidi na kuchangisha fedha ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wenye vimbe mbalimbali.
Related posts
Share this post
0 comments: