NATASHA AUGUA DENGUE NA KULAZWA...."NILIHISI NAAGA DUNIA KIUKWELI LAKINI NILIWAHI KWENDA HOSPITALI, NIMEPATA TIBA, NIMERUHUSIWA"
Posted in
No comments
Monday, May 12, 2014 By Unknown
STAA mkongwe wa filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ ameongeza listi ya mastaa ambao wameathirika na ugonjwa wa dengue (Dengue Fever).
Akiongea na mwandishi wetu, Natasha alisema tangu Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani, hajawahi kuugua hata homa lakini kwa mara ya kwanza mwaka huu homa ya dengue imemlaza.
“Nilianza kusikia baridi kali sana kisha nikawa naishiwa nguvu na mishipa inakakamaa, nilihisi naaga dunia kiukweli lakini niliwahi kwenda hospitali, nimepata tiba, nimeruhusiwa na ninaendelea vizuri,” alisema Natasha.
Miongoni mwa mastaa ambao wameumwa ugonjwa huo ambao hauna tiba ya moja kwa moja ni Rehema Chalamila ‘Ray C’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na Miss Afrika Mashariki namba 2, 2008, Aneth John.
Related posts
Share this post
0 comments: