PICHA ZA MWANAMKE ALIYEPIGA MAGOTI AKIOMBA DAWA ZA MAUMIVU HOSPITALI KABLA YA KIFO CHAKE.
Posted in
No comments
Friday, May 30, 2014 By Unknown
Unaweza kudhani matukio haya hutokea katika hospitali za kawaida tu.
Hii ni ya kusikitisha zaidi na imetokea katika hospitali kubwa nchini
Uingereza. Picha hii ya mwisho inamuonyesha mwanamke mmoja aliyekuwa
amezidiwa hospitali na akashindwa kupatiwa dawa hadi kuamua kupiga
magoti hospitali akibembeleza apatiwe dawa ya maumivu tu kutokana na
kuzidiwa kwake lakini wauguzi hawakumsaidia chochote hadi umauti
ulimkuta.
Siku mbili baada ya kutelekezwa na maafisa wa hospitali, mwanamama
huyo Margaret Lamberty alipoteza maisha baada ugonjwa wake unaotibika
kumzidi kutokana na kushindwa kupatiwa msaada.
Margaret alifikishwa hospitali ya chuo kikuu cha A&E North
Staffordshire nchini Uingereza na wanafamilia yake akiwa na maumivu
makali ya tumbo, Mtoto wake kike aitwaye Laura amesema kuwa baada ya
kufika hospitalini hapo wauguzi walikuwa wakimuangalia tu bila kumpa
msaada wowote ndipo mama yake akaamua hadi kupiga magoti akiwaomba
wampatie dawa ya maumivu lakini hakusikilizwa na mtu.
Hospitali hiyo imekumbwa na kashfa kubwa kwa sasa baada ya kifo cha
mwanamke huyo ambapo familia inapanga kuishtaki kwa kushindwa kutimiza
wajibu wao hadi kusababisha kifo cha ndugu yao.
Related posts
Share this post
0 comments: