BIASHARA MPYA YA DAVID BECKHAM, KUFUNGUA MLOLONGO WA MIGAHAWA
Posted in
No comments
Monday, June 9, 2014 By Unknown
Nyota wa zamani wa soka duniani David Beckham ambaye pia anatarajia
kujenga uwanja wa mpira utakaokuwa na uwezo wa kuingiza watu elfu 25
huko Miami, sasa amekuja na biashara mpya atakayoipa jina la ‘Beckham’s
Bistro’, kwa kujenga migahawa mingi.
Beckham mwenyewe anasema hiyo itakuwa kwa ajili ya mitoko ya vyakula tu kwani yeye ni mpenzi wa chakula.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 na mke wake Victoria wanaangalia
uwezekano wa kupanua hisa za biashara zao nchini Marekani ambapo tayari
wana urafiki na chef Gordon Ramsay, ambaye anamiliki migahawa mitatu
mjini Vegas.
David, ambaye ana watoto watano Brooklyn, 15, Romeo, 11, Cruz, 9, na
mtoto wao wa miaka miwili Harper na mke wake Victoria, waliripotiwa
kuwekeza katika moja ya migahawa mikubwa jijini London mwaka jana wakiwa
na mawazo tofauti.
Related posts
Share this post
0 comments: