HARRISON FORD APATA AJARI AKIREKODI FILAMU HUKO MAREKANI
Posted in
No comments
Friday, June 13, 2014 By Unknown
Mcheza filamu mkongwe wa nchini Marekani Harrison Ford anapatiwa matibabu hospitalini kutokana na majeraha aliyopata wakati akirekodi filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Star Wars.
Harrison Ford mwenye umri wa miaka 71 amevunjika kifundo chake cha mguu baada ya mlango wa eneo la kutengeneza magari kumuangukia wakati wakirekodi filamu katika studio za Pinewood nchini Marekani.
Mwigizaji huyo wa Hollywood ambaye ameigiza katika filamu ya Star Wars ambapo sasa anarekodi sehemu ya saba ya mwendelezo wa filamu hiyo alikimbizwa hospitalini ambapo msemaji wa kampuni ya kutengeneza filamu amesema wataendelea kurekodi kama kawaida.
Filamu hiyo inaigizwa na wasanii wenginge wakubwa kama Lupita Nyong’o, John Boyega, Daisy Ridley, Adam Driver, Oscar Isaac, Andy Serkis, Domhnall Gleeson, na Max von Sydow.
Tukio hilo limetokea wakati wa mwendelezo wa sehemu ya saba ya war Stars ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.
Related posts
Share this post
0 comments: