Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

MASANJA ASEMA HATOPOST PICHA ZA MISIBA TENA.

Posted in
No comments
Wednesday, June 11, 2014 By Unknown



Kupitia F/B Masanja Mkandamizaji ameandika hivi:


"Naona kuna watu wanahoji kwa nini siweki picha za misiba inayotokea ya ndugu zetu wasanii wa Bongo Movie. Jibu ni kwamba maisha ni mipango na maamuzi. Niliamua sitaweka picha za misiba katika mitandao ya kijamii kwa sababu kiuhalisia hazisaidiii chochote kwa yule aliyetutoka na hata faraja kwa ndugu, familia na marafiki zake. 


Nachojua ni kwamba mambo kama haya yanapotokea ni kumshukuru Mungu kwa yote, tena kwa faragha na kutoka moyoni mwako na sio kumshukuru kwa kuposti mapicha kwenye mitandao ya kijamii, tena wengine kwa kumdhalilisha hata marehemu kwa kuposti picha zisizostahili. Kwa hiyo basi niwaombe woooote mliokuwa mnasubiri niposti picha za misiba, siposti ng'oo! Kwanza hamna shukrani. 


Niliwahi kuposti mara moja na ya mwisho picha nikiwa kwenye msiba wa Ngwea mkasema oooh anauza sura msibani. Sasa nimeacha kuposti mnasema ooooh mbona hashiriki. Nyau kabisa! Na kwa taarifa yenu misiba yote ambayo ilitokea nikiwepo nilihudhuria na ambayo sikuwepo nyumbani nilitoa pole na kwenda kuwaona ndugu na familia za ndugu waliotutangulia niliporudi. Sitaweka picha za aina hiyo hapa. 


Hapa ni mwendo wa makomedi, mastetasi, majoksi, n.k. Kama ulini-like ili uwe unapata picha za msibani chapa mwendo. Eti oooh, kioo cha jamii (huku umebana pua), kabla hujaniita kioo cha jamii kumbuka na mimi ni binadamu na nina feelings na nasoma comments zenu na nina maamuzi yangu. Nimefinishi mwanawane senki yu veri machi"

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.