MREMBO WA KENYA MWENYE UMBO LA UTATA CORAZON KWAMBOKA, AKIRI KUMZIMIA HERMY B.
Posted in
No comments
Sunday, June 1, 2014 By Unknown
Kama girlfriend wako akikuona unaongea na Corazon Kwamboka, hakuna shaka kuwa roho yake itamdunda kwakuwa wazo la kwanza litakalomuijia kichwani ni kuwa himaya yake ipo matatani. Corazon Kwamboka ambaye ni mwanasheria by profession, ameiteka blogsphere ya Kenya kwa umbo lake matata na kuvutia kama la Agnes Masogange.
Hii imewafanya wasichana wengi wa Kenya wamuonee wivu na kumsema vibaya. Pamoja na kuwatoa wanaume udenda kwa umbo lake, producer wa B’Hits, Hermy B, amekuwa mwanaume mwenye bahati kwakuwa amezimiwa na mrembo huyo aliyeamua kuweka wazi kwenye Instagram.
“Before Monday ends.. here is my real crush #MCM. Hermes tpf,” aliandika mrembo huyo Jumatatu hii.
Related posts
Share this post
0 comments: