DIAMOND ATAMKA KUWAPA BARAKA ZOTE WALE WOTE WANAOTUMIA SURA YAKE KATIKA KUJITANGAZA.
Posted in
No comments
Thursday, July 17, 2014 By Unknown
‘Diamond Platinumz’ ni jina ambalo linakubalika zaidi ama jina la msanii wa bongo flava mwenye mashabiki wengi zaidi nchini Tanzania, lakini umati wa mashabiki wanaompenda Diamond ni soko la wajasiriamali ambao wanalitumia kuingiza siku.
Hivi sasa wapo wafanyabiashara wanaouza fulana zenye jina au picha ya Diamond bila makubaliano yoyote na msanii huyo.
Hata hivyo, wafanyabishara hao hawatakiwi kuwa na hofu. Mwimbaji huyo amefunguka katika kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm na kuwapa ruhusa wale wote wanaofanya hivyo.
“Kuwekwa tu pale kwangu mimi nimefurahi, nisiwe mnafiki. Siwezi kusema nimesikia uchungu eti kwa nini ametumia sura yangu hivyo. Yaani nimefurahi kwa sababu ninaona kama taifa limeni-appreciate kazi yangu na mtu katengeneza t-shits na kauza imeuzika kweli kwa sababu inaweza kuwekwa bwana ‘Salamu’ isiuzike (kicheko)…..mimi kwangu ni rukhsa” Amesema.
Ruhusa hii imepekwa hadi kwenye saloon.
Hata hivyo, ametahadharisha kutotumia brand ya ‘Wasafi Classic’ kwa sababu hiyo ni brand yake. “Labda mtu atumie ‘Wasafi’, hapo tatizo lingine.”
Related posts
Share this post
0 comments: