Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

DR. SLAA ADAI AKIWA MADARAKANI NA KUTUMIA DOLA, ATARUHUSU UTENGENEZAJI WA POMBE AINA YA GONGO KISHERIA

Posted in
No comments
Saturday, December 14, 2013 By Unknown

Default DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

Saturday, 14 December 2013 ·

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.

CHANZO: NIPASHE

NA JE, WADAU WAMEONGEA NINI KUHUSU HII HABARI YA KUTAKA KURUHUSU UENDESHAJI WA BIASHARA YA GONGO KAMA ILIVYOELEZWA NA DR. SLAA. 

 "hata kama anayechochea wananchi kufanya vurugu awe na mapembe marefu kiasi gani, atakamatwa na kukatwa hayo mapembe yake"

  1. #2

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Naona babu sasa amegeuka kuwa ze komedy

    Mimi nitaongea na kina Mpoki wamchukue kwenye show zao , atafaa sana
    ZeMarcopoloRuttashobolwaMsolwa and 2 others like this.
    JITAMBUE!

    Chadema kufikiri kuwa watachukua nchi ni sawa na yule jamaa alieota anataga mayai, alipoamka akajikuta ameachia mwakimba kitandani.
  2. Ritz is offline 
    #3

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Hali mbaya kwa Dr.Slaa baada ya kuona albamu yake ya ufisadi imefulia sasa kaamua kutoka ni single ya Gongo.
  3. #4

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Nchi ya Tanzania Mapato yake asilimia kubwa ni yanatokana na POMBE na TUMBAKU!

    Tafakari!
  4. #5
    TECH WIZ's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Haya kazi kwenu Great Thinkers!Inawezekana kweli hiyo au just political gimick?

  5. Ritz is offline 
    #6
    Ritz's Avatar
    JF Gold MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Ni wazo zuri nadhani makamanda wa Arusha watapata ajira ya kuuza gongo.
    NgongosekeRuttashobolwa and nderumo1962 like this.
  6. #7
    white girl's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Hahahahahahahahahaha mi naomba babu aruhusu na bangi kabisa siku akikamata hiyo dolaa
    The Fixer and Ruttashobolwa like this.
    Farasi umpandae hakutishi kwa mbio zakee
  7. #8
    nguvumali's Avatar
    JF Gold MemberArray

    Default

    Quote By Chris Lukosi View Post
    Naona babu sasa amegeuka kuwa ze komedy

    Mimi nitaongea na kina Mpoki wamchukue kwenye show zao , atafaa sana
    ni wajinga wa kariba yako wanaweza kufikiri sawa na upunguani wako
    ....poor

    ni wajinga
  8. ifweero is offline 
    #9
    ifweero's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Quote By anophelesi View Post
    Nchi ya Tanzania Mapato yake asilimia kubwa ni yanatokana na POMBE na TUMBAKU!

    Tafakari!
    Kwa hiyo unadhaurije mkuu, is slaa right?
    "hata kama anayechochea wananchi kufanya vurugu awe na mapembe marefu kiasi gani, atakamatwa na kukatwa hayo mapembe yake"
  9. #10
    sixgates's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Nadhani anathibitisha kuwa hiki chama cha wanywa viroba. Hivi huyu dokt ndie alitaka kuwa rais??
    Ruttashobolwa likes this.
  10. #11
    mwekundu's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Dah...ndo mana machalii wa Arusha wanalewa sana viroba,kumbe hizi ni baraka kutoka kwa #lema na #slaa ?
  11. ifweero is offline 
    #12
    ifweero's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Quote By nguvumali View Post
    ni wajinga wa kariba yako wanaweza kufikiri sawa na upunguani wako
    ....poor

    ni wajinga
    Taratibu mkuu, huku ni jukwaa la siasa sio matusi. Mpige kwa hoja uone km atanyanyuka
    Mahesabu likes this.
    "hata kama anayechochea wananchi kufanya vurugu awe na mapembe marefu kiasi gani, atakamatwa na kukatwa hayo mapembe yake"
  12. #13
    ZeMarcopolo's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Hahahahaha hii kali.

    Yaani kukamatwa na silaha kiwe kigezo cha mtu kupewa ajira!!! Kijana akikosa ajira anajikamatisha na silaha haramu halafu anapewa ajira!

    Tuliwaambieni kuwa Slaa ni mwanasiasa mlaghai, sasa mnaona? Kapokewa na kikundi cha wauza gongo anaona awalaghai kwa kuitetea gongo!
    "To greed, all nature is insufficient"
  13. ifweero is offline 
    #14
    ifweero's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Quote By mwekundu View Post
    Dah...ndo mana machalii wa Arusha wanalewa sana viroba,kumbe hizi ni baraka kutoka kwa #lema na #slaa ?
    Usitulaumu mkuu, hapo ndio uwezo wetu wa kufikiri umeishia, unadhani tutapataje kura za wapika gongo?
    "hata kama anayechochea wananchi kufanya vurugu awe na mapembe marefu kiasi gani, atakamatwa na kukatwa hayo mapembe yake"
  14. #15
    Apolinary's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Hata kama ni Bangi ikitungiwa Sera na Ikachambuliwa Vizuri itakua ni vema kuliko kukataza wakati kuna namna ya Kuitengeneza.
    Hongera Chadema kwa Uchambuzi Mzuri.
  15. #16

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Tofauti ya gongo na konyagi ni urasimishaji na kulipia kodi. Wajanja wameliona hilo wakaiweka kwenye packet wakaita viroba, wakalipa kodi ikaondolewa kwenye kundi la haramu. Binafsi sioni tatizo hapo
    Dark CityDingswayoKagalala and 2 others like this.
  16. ifweero is offline 
    #17
    ifweero's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Quote By ZeMarcopolo View Post
    Hahahahaha hii kali.

    Yaani kukamatwa na silaha kiwe kigezo cha mtu kupewa ajira!!! Kijana akikosa ajira anajikamatisha na silaha haramu halafu anapewa ajira!

    Tuliwaambieni kuwa Slaa ni mwanasiasa mlaghai, sasa mnaona? Kapokewa na kikundi cha wauza gongo anaona awalaghai kwa kuitetea gongo!
    Mkuu, ndio mana inaitwa siasa. Unacheza tu na akili za watu
    Mahesabu likes this.
    "hata kama anayechochea wananchi kufanya vurugu awe na mapembe marefu kiasi gani, atakamatwa na kukatwa hayo mapembe yake"
  17. ifweero is offline 
    #18
    ifweero's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Quote By Apolinary View Post
    Hata kama ni Bangi ikitungiwa Sera na Ikachambuliwa Vizuri itakua ni vema kuliko kukataza wakati kuna namna ya Kuitengeneza.
    Hongera Chadema kwa Uchambuzi Mzuri.
    Pole sana mkuu. Hivi binadamu ana miguu mingapi, sita ee?
    "hata kama anayechochea wananchi kufanya vurugu awe na mapembe marefu kiasi gani, atakamatwa na kukatwa hayo mapembe yake"
  18. Kibuja is offline 
    #19
    Kibuja's Avatar
    Senior MemberArray

    Default Re: DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

    Gongo=viroba, kwani viroba vinauzwa mafichoni? Msimuonee wivu dr kwa ubunifu wa ajira
  19. #20
    Ng'wanangwa's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray

    Default

    Quote By Ritz View Post
    Hali mbaya kwa Dr.Slaa baada ya kuona albamu yake ya ufisadi imefulia sasa kaamua kutoka ni single ya Gongo.
    SLAA kiboko ya magamba

Similar Topics

  1. Replies: 1
    Last Post: 4th March 2013, 13:13
  2. Replies: 25
    Last Post: 27th November 2011, 14:06
  3. Tetesi: Dr. Slaa na Chadema wajiandaa kukamata hatamu za dola na uongozi wa Taifa...
    By Rutashubanyuma in forum Tanzania 2010-2015
    Replies: 5
    Last Post: 16th October 2010, 23:33

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.