Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

CHUNGU CHA AJABU CHAIBUKA NA KUTOA DAMU JUU YA KABURI

Posted in
No comments
Monday, April 7, 2014 By Unknown

MAUZAUZA yametokea katika kaburi  la mtoto Agnes Mlawa (8) mkazi  wa Ilala  katika Manispaa ya  Iringa aliyezikwa mwaka  jana baada ya baba  wa  mtoto  huyo kukuta chungu cha ajabu chenye damu, maini na kichwa cha ndege kaburini hapo.

Tukio  hilo la aina  yake  limetokea leo majira ya saa mbili asubuhi  katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa wakati  baba mzazi wa mtoto  huyo Bw. Mlawa akichembua kaburi  hilo na mara  baada ya  kumaliza ghafla alishuhudia tukio hilo la chungu cha ajabu kuibuga juu ya kaburi hilo.

"Mimi nilikuja hapa kusembua kaburi la mwanangu ila baada ya kumaliza ghafla nilikuta kama damu  zinaruka juu kutoka kaburini na baada ya kuchunguza ndipo nilipoona chungu hicho kikiibuka juu ya kaburi "


Alisema  kuwa chungu  hicho kilikuwa  kimefunikwa na kitambaa cheusi juu ambacho kililowa dawa na kufungwa kamba ya nguo ya kijani na kutokana na  tukio hilo la ajabu alilazimika  kuacha jembe  juu ya kaburi na kukimbia  kuita watu wanaopita barabarani  ili kuomba msaada.

Mzazi huyo anadai kuwa  mazingira ya kifo cha mtoto wake yalikuwa ni ya kushangaza  baada ya  kuugua kwa  muda wa siku nne pekee na kufariki dunia.

Hata  hivyo alisema  kwa  kuwa kwa upande wake haamini mambo ya kishirikiana hakuona sababu ya  kumwita mganga wa kienyeji kwa ajili ya kushughulikia zoezi la kuchoma chungu hicho na badala  yake  kuamua kuifanya kazi hiyo mwenyewe hasa akiamini katika nguvu ya Mungu.


"Napenda kuwashukuru wananchi waliofika hapa kwa kunitia  nguvu na  pia kuwashukuru madereva  bodaboda akiwemo kijana Ahmed kwa kujitolea mafuta ya petroli kwa ajili ya kukichoma chungu hiki "

Mbali ya mzazi huyo kujitolea kuchoma chungu hicho na kuteketeza vitu vilivyokuwemo ndani, wananchi  waliofika kushuhudia tukio hilo walilazimika kutimua mbio wakihofia zoezi hilo la uchomaji wa chugu.

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.