Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

SULUHISHO LA WATU WALIO NA AIBU HASA WANAPOHITAJI KUTENDA MAMBO YENYE MANUFAA KWA WATU WAO WA KARIBU.

Posted in
No comments
Tuesday, December 31, 2013 By Unknown

 
Watu wenye aibu ndani yao wanafahamu fika kuwa kuna mambo mazuri yanawapita lakini wanahisi hawana jinsi ya kubadilisha hali hiyo.
  
Aibu kimahesabu ni sawa na:

AIBU = KUKOSA FURSA + KUKOSA FURAHA + KUFAHAMIANA NA WATU WACHACHE

Aibu ni kizuizi kikubwa sana kwa mwenye nayo kufikia mambo mazuri katika jamii.
Lakini naomba nikuambie hata kama wewe ni mmoja wao kuanzia leo 
unaweza kubadilisha hali hiyo kwa kutumia hatua zifuatazo:

1.MTAZAMO WAKO JUU YA WATU WENGINE

Watu wenye aibu mara nyingi wanajaribu kujitofautisha na 
watu wapya wanaokutana nao na kuwapa hadhi inayowazidi wao.
Hali hiyo itakufanya ujione huna jipya la kumueleza au kuzungumza mbele ya watu hao.
Unachopaswa kufanya ni 
kumuona kila mtu mpya unayekutana naye kama wa kawaida na hana alichokuzidi na kwamba hata yeye kuna vitu hajui 
au hana ambavyo wewe unavyo.

2.TAMBUA HATA WENGINE WANA AIBU PIA

Usijiweke peke yako kama ndio mtu mwenye aibu kupita wote na kwamba wengine 
hawako kama wewe.
Kuanzia leo tambua kuwa kila mtu ameumbwa na aibu ndani yake pale anapokutana na mtu mpya kwahiyo ukiwa 
mbele ya watu wapya 
jua hata wao pia wanakuonea aibu kwa kuwa hawajui ulichonacho ni nini.

3.KUSANYA TAARIFA NYINGI KICHWANI

Mtu mwenye aibu siku zote hujiona hana chochote cha maana 
kuwashirikisha wengine.
Kuna wengine wanakuwa kweli hawana vitu vya kuzungumza mbele za watu wengine na kuna wengine ni 
kujidharau tu na kuona taarifa walizo nazo hazina maana.
Jaribu kuwa na tabia ya kusoma vitu vipya na kuwaeleza watu wengine 
na hapo utafanya uwezo wako wa kusimama au kujitokeza mbele ya watu wengine kuwa mkubwa kwa kuwa kichwani 
una kitu cha kuwashirikisha.

4.ONGEZA KUJIKUBALI

Ukiwa na tabia ya kujidharau mwenyewe na kujiona huna thamani 
mbele ya wengine utafanya aibu ikuteke 
daima.
Thamini uwezo wa pekee 
ulionao na upe thamani kuwa hakuna mwengine alionao kwahiyo hata wewe 
unaweza kuwaonyesha maajabu wasiyoyajua.
Ukijiweka katika kundi 
hili hautakuwa muoga wa kuwasiliana 
na watu wapya kila siku.

5.ACHA KUZIAMINI HISIA HASI

Mtu mwenye hofu siku zote anatengeneza hisia ndani yake kuwa baada
 ya yeye kufanya au kusema jambo fulani
 basi watu wengine watafanya
 kitu fulani kwake.
Mathalani anaweza akaanza kuhisi kuwa baada ya yeye kukosea kitu 
watu watamcheka au kumsema vibaya
 kwa wengine.
Na anapoiamini hiyo picha kichwani kwake anaongeza aibu na kushindwa kuitumia fursa iliyopo mbele yake.
Na mara nyingi hizi hisia huwa hazina ukweli wowote katika matukio
 halisi ila ni hofu tu anayojijengea mwenyewe.
Anza kujitengenezea hisia chanya kuwa watu watakupongeza kwa kujaribu.

KUMBUKA;
AIBU HUWEZA KUKUFANYA UKASHINDWA KUTIMIZA NDOTO NA AZMA YAKO KATIKA MAMBO YAKO MBALIMBALI. HIVYO USIRUHUSU AIBU IWE KIKWAZO KATIKA KUTIMIZA NIA NA MALENGO YAKO, KWANI HUWEZA KUKUFANYA UONEKANE MTU ASIYE NA MSAADA NA ASIYE NA MANUFAA MBELE YA WALE UNAOWAJARI NA KUWATHAMINI.

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.