Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

DIAMOND AWAKERA WAISLAM BAADA YA KUCHEZA NGOLOLO MAULID

Posted in
No comments
Friday, March 28, 2014 By Unknown

Msanii nguli wa mziki wa bongo flava kutoka Tanzania maarufu kwa jina la Diamond, amewakera waislam wenzake waliohudhuria katika maulid ambapo tukio hilo liilihusisha kumtoa nje mtoto wa dansa wake aitwaye Moze Lyobo maeneo ya Mbagala, jijini Dar.

Nasib Abdul 'Diamond' akicheza dufu 'kingololo'

Awali watu waliokuwepo eneo hilo walifurahia uwepo wake lakini kadiri walivyoaanza kugundua kasoro ndipo mambo yalipoanza kuharibika.

“Watu hawakumshtukia, lakini walipomkagua kwa makini na kugundua licha ya kuvaa mavazi ya
Kiislamu ndani yake ana macheni ya dhahabu shingoni kitu ambacho dini hairuhusu,” kilidai
chanzo baada ya mwandishi wetu kufika eneo la tukio na kukuta shughuli imeisha.

Kama hiyo haitoshi, ikaelezwa kuwa Diamond alizidi kuchafua hali ya hewa baada ya kucheza
staili ya Ngololo kwenye kaswida kitu ambacho kiliwashangaza wengi.

“Mwanzo alianza vizuri lakini kadiri dufu lilivyokuwa linakolea, akawa anajisahau na kucheza
Ngololo, kimsingi aliwaboa baadhi ya Waislamu waliokuwa pale,” alisema shuhuda wetu.
Hata hivyo paparazi wetu alitonywa kuwa, baada ya kucheza sana, Diamond alichoka huku jasho
likimchuruzika ambapo aliamua kupumzika na kuwaacha wengine wakiendelea.

Habari: specially

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.