Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

ALIYEMPATIA MASOGANGE MADAWA YA KULEVYA HUYU HAPA

Posted in
No comments
Tuesday, April 22, 2014 By Unknown


‘Video queen’ wa Kibongo, Agness Gerald, ‘Masogange’, amefunguka  kuwa aliyempa mzigo wa unga  na akakamatwa nao nchini Afrika Kusini, alikuwa amevalia kininja, hali iliyomfanya ashindwe kumtambua.

 Taarifa za uhakika kutoka vyanzo vyetu makini katika kikosi kazi cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya nchini (Task Force), zinasema kuwa  mwanadada  huyo alipofika katika nchi hiyo, alipigiwa simu na mtu ambaye hamjui aliyemwambia kuwa atapewa mzigo, hivyo ajiandae kuupokea.

“Alidai kuwa kuna mtu aliyevalia kininja alifika eneo alilokuwepo uwanjani pale ambaye hakumsemesha badala yake alimpatia mzigo wa unga ambao ulikuwa kilo 150 ambao hapa kwetu ni madawa ya kulevya na kuondoka kusikojulika,” kilisema chanzo.
 Kwa upande wake, Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana  na Madawa ya Kulevya nchini,  Godfrey Nzowa alipohojiwa na gazeti hili alithibitisha kuwa Masogange aliwaeleza polisi wa Afrika Kusini kuwa aliyempa unga ule ni mtu aliyekuwa amevalia kininja.

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.