MASAI NYOTAMBOFU AITEMA KAMPUNI YA AL-RIYAMY. SASA AAMUA KUJITEGEMEA. SOMA ALICHOKISEMA HAPA
Posted in
No comments
Friday, April 18, 2014 By Unknown
MCHEKESHAJI maarufu hapa nchini katika swaga za kimasai ambaye pia ni
mmiliki wa masainyotambofu.info Gilliady Severine Kahema 'Masai
Nyotambofu' Ameamua kuitema kampuni aliyokuwa na mkataba nayo ya
Al-Riyamy Pro ambayo hurusha kipindi chake cha VITUKO SHOW kwenye
runinga ya CHANNEL TEN.
Akizungumza na Udaku Specially leo, Masai Nyotambofu alisema kuwa
ameamua kuachana na kampuni hio baada kugundua kuwa kuendelea kuwepo
pale kwa muda mrefu ni sawasawa na kuididimiza sanaa yake kwani hamna
mafanikio yeyote zaidi ya kuahidiwa kwamba baada ya kipindi fulani mambo
yatakuwa mazuri huku siku zinazidi kwenda, ''Kiukweli nimeamua kuachana
na Al-Riyamy Pro maana naona muda wote wa miaka mitano sijafikia
malengo yangu niliotarajia na ahadi za kampuni hazionekani,
Pia kikubwa zaidi kilichoniondoa ni pamoja na kuchezeshwa na wasanii
wasio na vipaji halisi wanaishia kuigaiga stile za watu tu hatima yake
tunaonekana wote wabovu. Hapo mwanzo tulivyokuwa timu kamili tulifanya
vizuri na kupokelewa vizuri lakini walivyoondoka baadhi ya wasanii wenye
uwezo mkurugenzi akasema analeta wasanii wengine, Basi mimi nikaendelea
kusubiri maana kila msanii alikuwa na mkataba wake hivyo kila
aliyeondoka aliondoka kwa sababu zake binafsi mimi nikaendelea kukomaa
nikihisi mbele ya safari kutakuwa na mabadiliko, Mara mkurugenzi akaaza
kuwaleta watu tu from no whwre wasio na vipaji vya sanaa tucheze nao,
Kila nikimuuliza kuwa mbona wengine wakisimama mbele ya Camera
wakiambiwa Action hawajui itakuwaje? Jibu lake alinijibu nawasaidia
maisha yao magumu.
Nikamwambia huoni kuwa kazi ikiwa mbovu tutapoteza
mashabiki? Akajibu we fanya kazi ntapitisha mchujo wasio na vipaji
ntawaondoa watabaki wenye vipaji wachache tu niwatengenezee maisha ili
muuone umuhimu wa kukaa kwenu hapa miaka mingi mimi nauona uvumilivu
wenu,
Cha ajabu mkurugenzi aliendea kujaza watu wasio na vipaji uongozi hakuna
nidhamu kambini mbovu mimi siheshimiwi na mimi simuheshimu mtu basi
tafrani kama kilabu cha komoni. Lakini nikaendelea kukomaa nikitarajia
mabadiliko mwaka 2014, Kuna siku nikajaribu kumwambia mkurugenzi kuwa
aniazime kiasi fulani cha fedha nikamilishe Video ya wimbo wangu alafu
anikate akasema sina hela huoni mko wengi? kwanza kampuni hainilipi wewe
unataka upate promo ili uzidi kuitwa kwenye Show utashuti saa ngapi na
kwenye Show utaenda saa ngapi? Dah!
Hapo ndipo nilipoona kuwa napoteza muda ukizingatia mwanzoni tulivyokuwa
wakali watupu kipindi kikiruka hewani simu za wasanii zinaita mpaka
kero lakini sasahivi kipindi kinaruka mwanzo mwisho hata hubipiwi..! Ni
ishara tosha kwamba watazamaji wameanza kuingia mitini. Ni bora nikae
pembeni nikinusuru kipaji changu kwani kama riziki yangu mwenyezi mungu
hakuniandikia kuipata hapo hata nikomae vipi kamwe sitofanikiwa hapo.
Nimeamua kurudi Nyumbani Jijini Dar kutuliza kichwa sina mkataba na
kampuni yeyote kwa sasa najiandaa kuachia ngoma mpya baada ile
niliyomshirikisha Rich Mavoko na Kitokololo (Yero Masai) Watu wangu
kaeni mkao wa kula Uchekeshaji siachi mpaka mwisho wa uhai wangu,
Kuondoka Al-Riyamy Pro Sio mwisho wa kampuni kufanya kazi wataendea
wengine na wala sio mwisho wangu wa kuchekesha bado mtaendela kuzipata
ladha zangu kupitia filamu zangu ambazo nipo katika mikakati ya
kuanzisha Project. Namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa kipaji hiki
kilichonifanya niwe na ukaribu wa hali ya juu na watu mbali mbali na
katika show zangu napokelewa vizuri hicho kinanifanya nimuheshimu kila
mtu wa kila rika, Nawapenda Mashabiki wangu One Love.
Related posts
Share this post
0 comments: